Mkamo wa pili wa rais
wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi amewataka wafanya biashara nchini kuwa na ushirikiano ili kuweza kujitangaza na kuongeza masoko ndani na nje ya
Zanzibar.
Balozi seif ametoa wito
huo wakati alipotembela wafanya biashara waliokuwepo katika tamasha la biashara
viwanda na masoko katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar.
Amesema katika
matamasha hayo yanaleta umoja kutokana na kukutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania
kwa upande wa wafanya biashara walifanya maenesho wa bidhaa zao katika tamasha hilo wamesema wamepata mafanikio makubwa tangu lilipoanza
tamasha hilo na kuiomba serikali kuwaongezea siku ili waendelee kufanya
biashara katika tamasha hilo.
Wakati huo huo waziri
wa biashara viwanda na masoko Zanzibar mh: balozi Amina Salum Ali akijibu ombi
la wafanya biashara hao amesema haiwezekani kuongeza muda wa tamasha hilo kutokana
na gharama zinazotumika katika viwanja hivyo.
Aidha amewataka wafanya
biashara hao kuwa wastahamilivu na kwamba maonesho yanayokuja watawekewa
utaratibu mzuri zaidi.
Mhe. balozi seif amefanya ziara katika tamasha la
biashara akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa mkoa wa mjini magharibi
mh: Ayoub Muhammed,mkuu wa wilaya ya mjini mh: Marina na viongozi wengine wa
serikali
Post a Comment