Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Visiwani Zanzibar Mh,
Ayoub Mohammed ameeleza kufurahishwa na ushiriki wa wananchi wa mkoa huo katika
kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar, sherehe
zilizofanyika kwenye uwanja Amani mjini Unguja.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mhe. Ayoub amesema kuwa wananchi wa mjini
magharibi wameonesha ushirikiano mkubwa na kuiunga mkono serekali ya awamu ya
saba chini ya uongozi wa Raisi wa Zanzibar na mweyekiti wa baraza la mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein.
Aidha ametoa
pongezi zake kwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa kuendelea kusimamia
sula zima la amani na utulivu nchini na kuhakikisha inaendelea kulindwa.
Shamra shamra za
miaka 53 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar zilianza December 31 mwaka jana na
kilele chake kilikuwa Alhamis.
Post a Comment