Waziri mkuu mstaafu
wa Ufaransa Manuel Valls amekashifiwa alipokuwa akihamasisha katika
kampeni za chama cha kisoshalisti katika uchaguzi mkuu wa kiti cha
Urais nchini Ufaransa.
Alipokuwa akihutubia katika ukanda wa
Magharibi mwa mji wa Brittany alipigwa kofi na kijana mdogo alipokuwa
akisalimia kwa kushikana mikono.
Mlinzi binafsi wa Bwana Valls alimkamata kijana huyo kooni kisha akamtupa chini.
Manuel Valls hajajeruhiwa katika tukio hili.
Post a Comment