WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka
Watanzania kutosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya
wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye
lengo la kupandisha bei za vyakula.
Amesema
Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo
na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli
wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani
hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)
kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya
upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya
habari.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali
vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli.
Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa
taarifa.
Amesema
baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari
wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.
Hata hivyo
Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo
mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda
mfupi yanayostahimili ukame.
Waziri
Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa
utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda
wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba
wa chakula katika nchi jirani.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula
nchini kwa sasa
Post a Comment