Mchezo wa bao ulioanza januari 13 mwaka wilayani Liwale-Lindi na kufikia tamati januari 16 kwa kupigwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Masula dhidi ya Kisimani mchezo uliokuwa mkali katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.
Katika mashindano hayo ya bao kulikuwa na jumla ya timu 12 yenye washiriki 48 kutoka sehemu mbalimbali wilayani Liwale.
Katika mchezo wa kwanza timu ya Masula iliyowakiahwa katika faili hiyo Nasoro Likecha iliweza funga goli namo dakika ya 2 na goli lilisawazishwa dakika ya 13 na Musa Mrope kutoka timu ya Kisimani.
Baada ya dakika 15 timu ya Kisimani ilipata goli la ushindi na kutwaa Mbuzi huku timu ya Masula ikishika nafasi ya pili ikijipatia Kuku 1.
Post a Comment