Umoja wa Wawakilishi wanawake
Zanzibar wamelaani vitendo vya
vya udhalilishaji wa
kijinsia vinavyoonekana kuongezeka Zanzibar ikiwemo ubakaji,
ulawiti na vipigo.
Mwakilishi
wa viti maalum Saada Ramadhan Mwendwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na
mwandishi wetu ambapo amesema watahakikisha vyombo vyote vinavyohusika na masuala ya
kisheria ikiwemo mahakama vinatenda haki kuona watuhumiwa wanaadhibiwa
kulingana na makosa waliyoyatenda.
Ameongeza kuwa kuna
umuhimu wa kuweka adhabu kali ili kuvitokomeza vitendo hivyo ambapo amesema
vikiachwa kuendelea vitaliangamiza taifa.
Aidha
amewasisitiza wananchi kuendelea kuitunza amani iliyopo nchini na kushirikiana
na Rais wa Zanzibar kuleta maendeleo nchini.
.
Post a Comment