Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi
Ayoub Mohammed amepiga marufuku uuzaji wa shisha katika mkoa huo akitaja
matumizi ya shisha kuwa ni chanzo cha uharibufu wa maadili kwa jamii ya
wazanzibar.
Mhe. Ayoub ametoa
marufuku hiyo katika hafla ya chakula cha watoto wenye matatizo ya akili
iliyofanyika katika skuli ya sekondari ya Ben Belle, amesema mahoteli, migahawa
na sehemu nyengine za starehe zinapaswa kuzuwia biashara hiyo na kufunga
kabisa.
Pamoja na hayo ameitaka
jamii kutokuwafungia ndani watoto wenye ulemavu hali aliyoitaja kuwa ni kitendo
cha udhalilishaji.
Post a Comment