CHAMA Cha
Mapinduzi CCM Zanzibar kimewaonya baadhi ya viongozi na wanachama
wanaowashutumu na kuwadhalilisha viongozi wenzao katika vyombo vya habari na
hadharani kinyume na utaratibu wa taasisi hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai ametoa kauli hiyo wakati akitoa mada ya
Muelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa CCM mwaka 2017/2022 katika mafunzo maalum ya siku
Moja ya viongozi na watendaji wa chama hicho ngazi za matawi, wadi na majimbo
ya Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja kichama.
Amesema
viongozi na wanachama wenye tabia hiyo ndani ya CCM hawawezi kuvumiliwa na
watachukuliwa hatua za kinidhamu kupitia vikao vya maadili vya chama hicho
endapo watathibitika kukutwa na hatia ya kuwajibika.
Nao Washiriki wa Mafunzo hayo waliwashauri viongozi
na Watumishi wa CCM na Jumuiya zake wa ngazi za Juu kuonyesha mfano wa
kiutendaji ili viongozi na wanachama wa ngazi za chini waweze kufuata nyayo
hizo kwa vitendo.
Mafunzo hayo ya siku
moja yamewashirikisha jumla ya viongozi na watendaji 487 wa chama na
jumuiya wa ngazi za matawi, wadi na majimbo ya Wilaya ya Kaskazini “B” kichama.
Post a Comment