Taasisi zinazohusika na
masuala ya kutoa elimu Zanzibar zimeshauriwa kuendesha mafunzo ya ujasiriamali
kwa jamii ya watu wenyeulemavu ili kuwatoa kwenye wimbi la utegemezi.
Akizungumza na waandishi wa habari Hadaa Khatib Simai ambae ni mwalimu katika chuo cha Upendo kilichopo Mwanakwerekwe visiwani Zanzibar kinachotoa elimu ya
ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu amesema hatua ya Serikali kuweka mkazo katika
ujenzi wa vyuo vya namna hiyo kutapanua wigo katika ushindani wa kibiashara.
Pamoja na hayo amesema
kumekuwa na changamoto ya ukosefu wa masoko jambo linalopelekea baadhi ya walemavu kuvunjika moyo katika kujiunga na chuo hicho kwa ajili ya kupata taalima ya ujasiliamali.
Post a Comment