0
 Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya kwanza Juma Kamkosa katika mchezo wa  kukuna nazi

 Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya kwanza Abasi Chonde katika mchezo wa mbio za baiskeli
 Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya pili Omari Robo katika mchezo wa mbio za baiskeli
  Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya kwanza Habibu Likecha katika mchezo wa bao
  Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya pili Mzee Mohamedi Masula katika mchezo wa bao
 Mratibu wa mashindi,Selemani Nangomwa (kushoto) akimkabidhi zawadi mshindi wa nafasi ya kwanza Juma Kamkosa katika mchezo wa  kukimbia na ndoo ya maji bila kushikilia (Picha na Liwale Blog)

Washindi 8 wa tamasha la michezo lililofanyika disemba 29 mwaka 2016 hadi januari 1 mwaka 2017 wamekabidhiwa zawadi zao mbalimbali januari 2 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa George’s club wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Tamasha hilo lilikuwa na lengo la kuuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017 lilihusisha michezo mbalimbali kama mbio za baiskeli,bao,kukuna nazi wanaume,kukimbia na ndoo ya maji kwa wanaume bila kushikiria na mchezo wa bao.

Mratibu wa mashindano hayo kaimu afisa utamaduni wilaya,Selemani Nangomwa aliwataja washindi hao katika shindano hilo ni;

Mchezo wa kukuna nazi kwa wanaume.
  1.       Juma Kamkosa 
  2.  Adamu Likwawatu
Mchezo wa kukumbia na ndoo ya maji bila kushikilia
  1.      Juma Kamkosa
  2.  Daudi Manjipa
Mchezo wa bao washindi
  1. Habibu Likecha      
  2. Mohamedi Masula
Mbio za baiskeli washindi
  1.     Abasi Chonde
  2. Omari Robo      
Mratibu wa mashindano hayo Nangomwa alisema kila mshindi kwa nafasi ya kwanza amezawadiwa fedha shilingi 20000 na mshindi wa pili shilingi 10000 kwa kila mchezo huku tamasha la michezo likidhamini na Bw. Hassani Mpako.

Baadhi wa washindi mara baada ya kukabidhiwa zawadi walizungumza na mwandishi wetu,Juma Kamkosa ambaye aliweza kushika nafasi ya kwanza mbili kwa mchezo wa kukuna nazi na kukimbia na ndoo ya maji alisema siri kubwa ya ushindi ni kujihusisha na michezo pia aliongeza kusema hata kabla ya mashindano hayo aliwahi kukuna nazi nyumbani kwake hili ilimasaidi sana kupata ushindi.

Kwa upande wake Mzee Mohamedi Masula alisema anajisikia faraja sana kushika nafasi ya pili kwenye mchezo wa bao huku akieleza michezo ni burudani hivyo amewaomba wadau wa michezo kujitokeza kushiriki kwenye mashindano mbalimbali kuacha kudhalau kile kinachoshindaniwa na kutakiwa kuthamini uwezo wao walionao na kuacha kubeza kinachoshindaniwa.

Post a Comment

 
Top