0
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili Olafu Mwageni na Bartazali Mwageni kwa tuhuma za kuchoma moto ofisi ya serikali ya kijiji cha Mtyangimbole halmashauri ya Madaba na kuteketeza nyaraka zote za serikali, 
Tukio hilo ni la tatu kutokea ndani ya mwezi mmoja kijijini hapo na kwamba gari la mwananchi mmoja na nyumba ya mwalimu iliteketezwa kwa moto hali inayo wafanya wananchi kuishi kwa hofu kubwa.
Mbunge wa jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama ametembelea kijijini hapo na kushuhudia nyara za serikali zikiwa zimeteketea kwa moto mwenyekiti wa kijiji cha Mtyangimbole amesema kuwa watuhumiwa hao wamelalamikiwa mara kadhaa kituo cha polisi kuwa wanashiriki vitendo viovu vya kuteka magari na kuyachoma moto wanapokamatwa wanaachiwa kabla ya kupelekwa mahakamani.
Kwa upande wake Mbunge wa Madaba Joseph Mhagama amelitaka jeshi la polisi kufanya kazi za wananchi wanapopokea malalamiko ya wananchi vema wakayafanyia kazi kabla ya waharifu hawajaleta madhara zaidi.
 Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma ACP Zuberi mwombeji amesema kuwa wanawashikilia watuhumiwa ambapo upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Post a Comment

 
Top