0

Wakulima wa kata ya Matekwe ambao korosho zao waliuzia karika chama cha msingi cha ushirika cha Mbondo(Mbondo AMCOS) wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi wamegoma kupokea malipo ya korosho zenye uzito wa tani 357,baada ya kutoridhishwa na mfumo uliotumika kuwalipa.

Mmoja wa wakulima hao,Haji Nanjase alisema ingawa wanatambua bei ya zao hilo iliyotangazwa na serikali ni shilingi 1300 kwa kila kilo moja.

Lakini wamekataa kulipwa shilingi 2500 kwa kila kilo moja kutokana na kutoridhishwa na namna korosho hizo zilivyonunuliwa.

Alisema korosho baadhi ya korosho wanaamini ziliuzwa au zingeweza kuuzwa katika mnada wa sita au wa saba,minada ambayo bei zake zilikuwa za juu.Hata hivyo zimeuzwa katika mnada wa nane.

Huku sababu za msingi zikiwa hazieleweki." Hata hivyo wapo waliolipwa bei kubwa ambao walipeleke baada ya sisi kupeleka na waliuza kwenye mnada wa saba na kulipwa bei mzuri,"alisema Nanjase.

Mkulima huyo alibainisha kwamba kufuatia hali hiyo walikwenda bodi ya korosho ambako walipata ufafanuzi wa taratibu zinazo tumika.

Nimaelezo ambayo wameridhika nayo na kuwasuma kwenda ngazi za juu."Kesho tunakwenda kuonana na mkuu wa mkoa wetu,tusiporidhika tutakwenda kwa waziri mwenye dhamana ya kilimo,"aliongeza kusema Nanjase.

Post a Comment

 
Top