Makamu wa Rais
mteule wa Marekani Mike Pence amesema mchakato wa kufutilia mbali sheria
ya afya iliyoanzishwa na Obama utaanza siku ya kwanza Donald Trump
atakapoingia madarakani.
Baada ya mkutano na wanachama wa
Republican na viongozi katika bunge la congress,Pence amesema Rais
mteule alikuwa anashughulikia sheria mahususi zinazohusika ili kuruhusu
mabadiliko kuelekea katika mfumo mpya wa sheria za afya.Lakini amesema mbivu na mbichi zitajulikana baada ya miezi kadhaa.
Msemaji wa serikali Paul Ryan amesema atahakikisha kwamba hapatakuwapo mtu yeyete atakayewaangusha.
Lakini kiongozi wa chama cha Deomocratic katika bunge la senati Chuck Schumer amesema chochote kilichotokea ni jukumu la Republican jambo ambalo ni wazi na rahisi.
Post a Comment