0

NA SELEMANI,ZANZIBAR

Mashabiki na wanachama wa Club ya Simba  Visiwani Zanzibar wanamatumaini makubwa ya kunyakua ubigwa wa kombe la mapinduzi kutokana na uimara  unaooneshwa na wachezaji wa kikosi chao.


Simba ya Dar es Salaam inatarajia kushuka dimbani kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Taifa Jang’ombe majira ya saa mbili za usiku katiak Uwanja wa Amanani Visiwani Zanzibar

Timu ya Taifa ya Jang’ombe  leo itashuka dimbani kwa mara ya pili kucheza na Simba huku ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kushinda kwa ujumla wa bao 1-0 katika uchezo wao wa mwanzo dhidi ya watani wao wajadi Jang’ombe Boys mchezo ambao umepigwa siku ya ufunguzi wa michuano hiyo  desembar 31 mwaka jana
Katika kuelekea mchezo huo mshabiki wa Simba  aliejitambilisha kwa jina la Omari  wa Tawi la Mlingotini Amani visiwani Unguja amesema matumaini yao kushinda mchezo huo wa leo na mechi nyenginezo na hawana wasi wasi na kikosi chao kwakua lengo lao ni kuchukua ubigwa wa kombe la Mapinduzi
“unajua Simba ni timu kubwa na wala huwezi kuifananisha na Timu nyengine yoyote hapa Tanzania hivyo sisi kama wanasimba kwa umoja wetu hapa Zanzibar tunamatuamini makubwa sana ya kunyakua ubingwa wa Mapinduzi hata wa Ligi kuu bara” alisema Omari
Nae makame Awadhi ambae pia ni mshabiki wa Club ya Simba Visiwani hapa amesema simba ni lazima ichukue ubigwa kutokana na uwezo unaooneshwa na wachezaji wake katika ligi kuu bara huku akimtolea mfano  Pastory Athanas mshambuliaji  chipukizi wa Simba waliomsajili katika kipindi cha dirisha dogo akitokea Stend United ya Mkoani Shinyanga

“ukweli ni kwamba Simba ndio timu bora zaidi hapa Tanzania,maana hata ukiangalia mchezaji mmoja mmoja wana vipaji vya hali ya juu tofauti na Yanga ambao wachezaji wao wengi wazee, embu angalia Yule kijana aliyetoka stend(Pastory Athanas) kacheza michezo miwili tu lakini ni moto wa kuotea mbali, sasa kama hivyo kweli hakuna kinachoizuiya Simba kuchukua ubigwa huu wa Mapinduzi  wala ligi kuu Tanzania bara” alisema Awadhi.

Simba ni miongoni mwa vilabu  vyenye rekodi nzuri ya michuano ya mapinduzi kuanzia mwaka 2007 ambao wamelichukua mara tatu mwaka 2008,2011 na 2015 ukilinganisha na yanga ambao wamelichukua mara moja ambao ni mmwaka 2007  huku azam ikichukuwa mara mbili 2012 na 2013
Angalia hapo chini nimekuwekea ratibiba ya mabingwa wa kombe la mapindizi linalofanyika kila mwaka Zanzibar
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
Mwaka     Bingwa             Mshindi wa Pili
2007         Yanga SC          Mtibwa Sugar
2008         Simba SC          Mtibwa Sugar
2009         Miembeni          KMKM
2010         Mtibwa Sugar   Ocean View
2011         Simba SC         Yanga SC
2012         Azam FC           Simba SC
2013         Azam FC           Tusker FC
2014         KCCA                Simba SC
2015         Simba SC          Mtibwa Sugar

2016         URA                   Mtibwa Sugar


Post a Comment

 
Top