Mjumbe
wa halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM Balozi Seif Ali Iddi
amesisitiza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha inatatua tatizo la
ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kujenga vituo viwili vya mafunzo ya amali
Unguja na Pemba.
Akifunga
matembezi yaliyoandaliwa na jumuiya ya vijana wa chama hicho UVCCM kuazimisha
miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kiswandui
mjini Unguja, Balozi Seif ambae pia ni makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar
amesema kujengwa kwa vituo hivyo itasaidia kutoa fursa kwa wananchi kujiajiri
wenyewe.
Awali mwenyekiti wa UVCCM Taifa mhe. Sadifa Juma ameiomba Serikali kutokuwavumilia watendaji wake ambao wameonesha kuyabeza mapinduzi matukufu ya Zanzibar hatua aliyoitaja kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Mapema akiwasalimia vijana zaidi ya 400 kutoka mikoa mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara walioshiriki matembezi hayo, waziri mwenye dhamana ya masuala ya muungano Mhe. January Makamba amewasihi vijana kuienzi CCM kutokana na msingi wa mapinduzi na muungano wa Tanzania kutegemea uwepo madarakani wa chama hicho.
makamo
wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhiwa picha ya raisi wa
kwanza wa Zanzibar Abed Amani Karume wakati akiwapokea vijana wa uvccm katika
kilele cha matembezi yao ya kuazimisha
miaka 53 ya mapinduzi.
Awali mwenyekiti wa UVCCM Taifa mhe. Sadifa Juma ameiomba Serikali kutokuwavumilia watendaji wake ambao wameonesha kuyabeza mapinduzi matukufu ya Zanzibar hatua aliyoitaja kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Mapema akiwasalimia vijana zaidi ya 400 kutoka mikoa mbalimbali ya Zanzibar na Tanzania Bara walioshiriki matembezi hayo, waziri mwenye dhamana ya masuala ya muungano Mhe. January Makamba amewasihi vijana kuienzi CCM kutokana na msingi wa mapinduzi na muungano wa Tanzania kutegemea uwepo madarakani wa chama hicho.
Kilele cha matembezi
hayo kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM na jumuiya zake akiwemo Naibu
katibu mkuu CCM Zanzibar Vuia Ali Vuai, makamo mwenyekiti UVCCM Mboni Mahita,
kaimu katibu mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka na kaimu naibu katibu mkuu UVCCM
Zanzibar Abdulghaffar Idrissa.
Post a Comment