0

Michuano ya mapinduzui Cup inaingia katika hatua ya nusu fainali hii leo kwa kupigwa michezo miwili tofauti majira ya jioni na usiku katika uwanja wa Amani Visiwani Zanzibar.
Mchezo huo wa mapema utawakutanisha matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam fc dhidi ya Taifa Jang’ombe (wakombozi wa ng’ambo ila katika hatua hii ni wakombozi wa Zanzibar) utakaopigwa jioni ya leo majira ya saa 10:30




 Ila macho ya wapenzi wengi wasoka visiwani hapa na Tanzania kwa ujumla macho na masikio yao  ni katika mchezo wa nusu fainali ya pili itakayopigwa majira ya saa 2:15 usiku utakaowakutanisha magwiji wa soka Tanzania Yanga na Simba zote kutoka mtaa mmoja wa Kariakoo, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa wapinzani wa jadi katika soka ya Tanzania utakuwa wa kwanza kuzikutanisha timu hizo visiwani humo tokea kukutana mara ya mwisho mwaka 2011.

Simba na Yanga zilikutana Januari 12, mwaka 2011 kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo ya Mapinduzi na Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-0 mabao hayo yaliwekwa kimiyani na Mussa Hassan Mgosi na Shijja Hassan Mkinna.

Katika Ardhi ya Zanzibar  Simba na Yanga zimekutana mara nne hadi leo na marazote hizo Yanga imeshinda mara moja mwaka 1975 kwenye fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mabao 2-0 ya Sunday Manara na Gibson Sembuli ambae kwa sasa hatunae Duniani.

Mechi nyingine tatu Yanga wamefungwa na mbali na hiyo ya 2011 ya Mapinduzi, walifungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1, Simba wakitangulia kwa bao la Hussein Marsha na wao kusawazisha kwa bao la Said Mwamba ‘Kizota’ (marehemu) na Nusu Fainali ya Ligi ya Muungano 1-0, bao pekee la Damian Kimti zote mwaka 1992.

Yanga inaingia kwenye mchezo wa leo, ikitoka kufungwa 4-0 na Azam FC katika mechi ya mwisho ya Kundi A Jumamosi, wakati Simba ilishinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys Jumapili.


Post a Comment

 
Top