0


Wakongwe wa kulitandaza soka Tanzania Bara  Simba na Yanga watakutana kesho Jumanne katika uwanja wa Amani katika hatua ya nusu fainli ya michuano ya mapinduzi Cup.
 
 Hatua ya mchezo huo utakaopigwa leo januari 10 majira ya saa 2:3o za usiku inafuatia baada ya Simba SC kushinda 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys mchezo ambao umepigwa jioni ya jana ikiwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi
Matokeo hayo yanaifanya Simba imalize kileleni mwa Kundi A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Taifa jang’ombe nafasi ya pili yenye pointi saba baada ya kushinda mchezo wake wa jana usiku dhidi ya mabigwa watetezi URA
Ikumbukwe Yanga imeshika nafasi ya pili Kundi B wakiwa na point sita  nyuma ya Azam  wanaaoongoza wakiwa na pointi saba
Kwa mlolongo huo yanga watalazimika kucheza na mshindi wa kwanza kundi A ambae ni Simba,huku Azam watashuka dimani kucheza na Taifa Jang’ombe Boys (wakombozi wa ng’ambo kutoka hapa visiwani Zanzibar).
Katika mchezo wa jana jioni , mabao yote ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo moja kila kipindi.

Mavugo aliyesajiliwa Simba SC msimu huu kutoka Vital’O ya kwao Burundi, alifunga bao la kwanza dakika ya 11  kwa shuti baada ya kuukuta mpira uliorudi baada ya kuogonga nguzo ya lango,
Mavugo akafunga bao la pili dakika ya 53 kwa shuti kali tena baada ya kupokea pasi ya Kichuya pembeni kulia na kumkokota beki wa Jang’ombe hadi kwenye 18 kabla ya kufunga.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Peter Manyika, Janvier Besala Bokongu/Vincent Costa dk78, Mohammed Hussein ‘Thabalala’,  Anbdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya/Hijja Ugando dk71, Muzamil Yassin/James Kotei dk46, Pastory Athanas, Laudit Mavugo/Jamal Mnayte dk55 na Juma Luizio/Moses Kitundu dk63.

Jang’ombe Boys; Hashim Ruga, Shomary Ismail, Muharami Issa, Ibrahim Said/Abubakar Ali dk72, Ali Badru, Yakoub Omar, Abdi Kassim, Khamis Makame, Hafidh Juma, Juma Ali/Ali Suleiman dk67 na Abdulsamad Ali.

Post a Comment

 
Top