Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa
Pili ya Rais Zanzibar, Mh Mohamed Aboud Mohamed amewataka wananchi kisiwani Pemba
kuzitumia fursa ziliopo ili kujiletea maendeleo mijini na vijijini.
Amesema zipo fursa nyingi ambazo
zinaweza kuwasaidia wananchi iwapo watazitumia vizuri kwa kushirikiana na
Serekali za Mikoa na Wilaya na kuacha vitendo vya hujuma miongoni mwao ambavyo
vinaweza vikaleta fitina ndani ya nchi.
Waziri Aboud ameyasema hayo wakati
akiweka jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Baraza la Mji Chake chake
ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambalo
linatarajiwa kugharimu sh million 944 na laki tatu hadi kukamilika kwake.
Nae Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa Idara Maalum SMZ Radhia Rashid amesema
lengo la kujengwa jengo hilo ni kuwawekea mazingira mazuri
wafanyakazi na kuwawezasha kufanyakazi zao kwa ufanisi zaidi .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa
Kusini Pemba Bi Mwanajuma Majidi Abdulla amewataka wananchi kuendelea
kushirikiana na Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani lengo la
serekali ni kuhakikisha maendeleo na kuleta ufanisi kwa
wananchi wake
Post a Comment