Raia nchini
Marekani bado wanaendelea na maandamano ya kupinga amri ya kiutawala
iliyotolewa na Rais Trump inayozuia kwa muda raia wanaotoka mataifa saba
ya kiislamu kuingia nchini Marekani.
Hata hivyo, tangu hatua
hiyo kutolewa, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa raia wa nchi
mbalimbali huku baadhi wakiunga mkono hatua hiyo, na wengine wakiipinga
vikali kwa kusema kuwa ni makosa watu kubaguliwa kutokana na imani zao
za kidini.Wakati huo huo, Kaimu mwanasheria mkuu nchini Marekani ameamuru idara ya wanasheria kutoitetea mahakamani amri hiyo.
Sally Yates, ambae aliteuliwa na Barack Obama, amesema bado hajashawishika kwamba inaruhusiwa kisheria.
Lakini msemaji wa Rais amewajibu kwa kuwaambia, wafuate amri hiyo au waondoke.
Nae aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama amevunja ukimya kwa kutoa taarifa inayosema amesikitishwa na maandamano yanayoendelea nchini humo.
Post a Comment