Yahya Jammeh
Vikosi vya nchi za
Afrika Magharibi vimemkamata kamanda mmoja wa cheo cha juu nchini
Gambia, na kupata silaha kweye makao ya kibinafsi ya rais wa zamani
aliye uhamishoni Yahya Jammeh.
Jenerali Bora Colley, mkuu wa kikosi maalum alikamatwa katika nchi jirani ya Senegal.
Vikosi vya kikanda pia vimevamia nyumba ya bwana Jammeh iliyo kijiji mwao eneo la Kanilai na kupata silaha.
Jenerai
Colley alikuwa kamanda wa zamani wa kambi ya jeshi ya Kanilai ambapo
Jammeh alikuwa na mpango wa kahamia akistaafu, kabla ya kulazimishwa
kukimbilia uhamishoni kwa kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa Disemba
mosi mwaka 2016.
Walinzi wanne wa mke wa Jammeh, Zainab, pia nao walikamatwa kwenye mji wa mpaka wa Karang nchini Senegal.
Vikosi
vya kikada vimekuwa vikimsadia Raia Adama Barrow kuchukua hatamu za
uongozi, katika taifa hilo dogo la Afrika Magharibi tangu bwana Jammeh
akimbilie uhamishoni zaidi ya wiki moja iliyopita.
Post a Comment