MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota
Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa
ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli
wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo
wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya
Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo |
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Baadhi
ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya
wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima
baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao
Hayo
wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika
katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya
Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai
(morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya
kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema
kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao
unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa
hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi
tangu enzi za mababu zao .
Mmoja
wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata
alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na
kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu
wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi
wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho
anatokea.
“Tumekuja
apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu
halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa
sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha
mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao
tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama waCCM hamna mwanachama hata
mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi
mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu
Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer
lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni
wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki
kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa
sana”alisema Amina Longitoti
Akiogea
katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya
ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya
wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na
chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.
Alisema
vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe
Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata
michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi
hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu
kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.
Alisema
CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa
halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi
wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi .
“mimi
nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa
shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha
kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na
kwakweli sita vumilia kabisa na kingine kinachonishangaza sio mimi tu
au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi
kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu
mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa
Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote
amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu “alisema Sanare
Kwa
upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai
alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo
unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema
linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala
hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa kwenda iwapo
wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao
Naye
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga,
aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma
kupitia
Hivi
karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Monduli,
lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa madai kuwa
waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa
wilaya hiyo.
Post a Comment