Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed S hein
leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali
katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu
Mjini Zanzibar ni Dk. Sira Ubwa Mamboya ambaye anakuwa Mjumbe wa Baraza la
Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum.
Wengine ni Bi Zainab Omar Mohammed ambaye anakuwa Mshauri wa Rais wa
Masuala ya Jamii, Wazee, Wanawake na Watoto, Dk. Maua Abeid Daftari anakuwa
Mshauri wa Rais- Pemba na Bi Rahma Ali Khamis ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu,
Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa
Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa
Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Said Hassan Said, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Issa Haji Gavu.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mawaziri wasio na Wizara
Maalum ambao pia, ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Naibu Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Shadya Mohamed Suleiman, Mufti
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji.
Na wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib
Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa
Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Sira Ubwa Mamboya kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi (BLM) na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum,katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 23/01/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Dk.Mauwa Abeid Daftari kuwa Mshauri wa Rais -Pemba katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjin Unguja,[Picha na Ikulu.] 23/01/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein akimuapisha Bi Rahma Ali Khamis kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ,katika
hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjin Unguja,[Picha na Ikulu.] 23/01/2017.
Post a Comment