Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kushirikiana na Urusi na China, iwapo mataifa hayo yatashirikiana naye.
Katika
mahojiano na Wall street journal, bw Trump amesema vikwazo
vilivyowekewa Urusi hivi majuzi, vitaendelea kuwepo, japo huenda
vikaondolewa iwapo Urusi itasaidia Marekani katika vita dhidi ya ugaidi.
Anatumai kwamba atakuwa na kikao na rais Putin hivi karibuni.
Pia amesema kuwa sera ya One China ambayo Marekani haitambui Taiwan itajadiliwa upya.
Wakati
huohuo kamati ya bunge la seneti nchini Marekani imetangaza kwamba
itachunguza madai kwamba urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
Post a Comment