0
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye ana umri wa miaka 36Eman Ahmed Abd El Aty mwenye ana umri wa miaka 36
Hospitali moja ya India inajenga kituo muhimu cha matibabu ambacho mwanamke mmoja wa Misri anayeaminika kuwa mzito duniani akiwa na kilo 500 atafanyiwa upasuaji ili kupunguza uzani wake.
Kituo hicho katika hospitali ya Mumbai ya Saifee kitakuwa na chumba cha upasuaji na kile cha wagonjwa mahututi.
Eman Ahmed Abd El Aty mwenye umri wa miaka 36 anatarajiwa kuwasili katika mji huo mwisho wa Januari.
Familia yake inasema kuwa ameshindwa kutoka nyumbani kwa takriban miaka 25.
Makadirio ya uzani wake hutolewa na ndugu zake.
Iwapo itathibitishwa atakuwa mwanamke mzito zaidi duniani aliyehai, kwani mwanamke anayeshikilia rekodi hiyo ya Guiness ni Pauline Potter wa Marekani ambaye ana uzani wa kilo 292 mwaka 2010.
Bi Abd El Aty atatibiwa na kundi la madaktari wanaongozwa na daktari wa upasuaji wa kupunguza matumbo kwa lengo la kutaka kupunguza uzani Daktari Muffazal Lakdawala.
  Mwanamke huyo atalazimika kupunguza uzani wake kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Mwanamke huyo atalazimika kupunguza uzani wake kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Kwa kuwa mgonjwa huyo hawezi kutumia ndege ya kawaida ,atasafirishwa hadi Mumbai katika ndege ya mizigo pamoja na dadake ambaye ndiye anayemuuguza, daktari mmoja katika hospitali hiyo ameambia mwandishi wa BBC Geeta Pandey.
Kwanza atalazimika kupunguza uzani wake kabla ya kufanyiwa upasuaji.
Bi Abd El Aty anaugua tezi na ugonjwa wa moyo na atalazimika kusalia hospitalini kwa takriban miezi sita ,daktari huyo amesema.
Ripoti zinasema chumba hicho kitagharimu Rupee milioni 20 na kitakuwa tayari mwishoni mwa mwezi huu.
Familia ya Abd El Aty inasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 5 alipozaliwa kabla ya kupatikana na ugonjwa wa matende, ugonjwa ambao unasababisha kufura kwa mwili kutokana na maambukizi ya vimelea.
Wakati alipofikisha umri wa miaka 11, uzani wake uliongezeka maradufu na akaugua kiharusi ugonjwa uliomuacha kitandani kwa kipindi kirefu cha maisha yake.
Mamake na dadake wanamuuguza.
  Je upasuaji wa kupunguza matumbo ni upi?
Je upasuaji wa kupunguza matumbo ni upi?
Hatahivyo daktari Lakdawala ameambia BBC mwezi uliopita kwamba anaamini bi Abd El Aty haugui ugonjwa wa matende lakini anaugua ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi ambao husababisha miguu kuvimba.
Ubalozi wa India mjini Cairo ulikuwa umemkatalia kupewa visa bi Abd El Aty kwa kuwa hakuweza kusafiri pekee.
Alipewa visa baada ya Dr. Lakdawala kutuma ujumbe katika Twitter kwa waziri wa maswala ya kigeni nchini India Sushma Swaraj ambaye alijibu kwa ombi la kutaka kutoa usaidizi.
Upasuaji wa kupunguza matumbo ili kupunguza uzani wa mtu aliye na uzani mkubwa hutumika kama hatua ya mwisho ya kuwatibu watu walio na uzani mkubwa na walio na mafuta mengi.

Post a Comment

 
Top