MTANDAO
maarufu wa kijamii WhatsApp upo katika harakati za kuwawezesha
watumiaji wake kufuta ujumbe uliotumwa kabla haujapokewa upande wa pili.
Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua
umefanya kosa katika WhatsApp, lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu
tayari umeshatumwa na kupokewa.
Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu zenye mfumo endeshi wa iOS.
Katika hilo kutakuwa na program katika eneo la ‘Settings’, ambapo
utatakiwa kue-‘Edit’ kisha ‘Revoke’ mchakato utakaowezesha kufuta ujumbe
huo kwa wakati mara tu unapogundua umekosea.
Hata hivyo, kikubwa ni kuwa utaweza kufanya hivyo kama tu uliomfikia
bado hajausoma, ikimaanisha iwapo ameshausoma hutaweza kuufuta.
Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.
Post a Comment