Rais wa Marekani
Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa
chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo
kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya
mataifa ya kiislamu.
Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti.
Sally
Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba
marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali.
- Trump: Wakimbizi wa Syria hawaruhusiwi Marekani
- Trump ajitetea kuhusu sera ya usafiri
- Sudan yapinga amri ya Trump
- Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?
Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente.
Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni.
Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Post a Comment