
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na wamiliki wa Bloggers Tanzania kabla ya kufunga mafunzo kwa mablooger
hao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufungaji wa
wa mafunzo kwa mablooger Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers network Bw. Joachim Mushi
akizungumza na wamiliki wa Bloggers Tanzania kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye
kufunga mafunzo kwa Bloggers Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimkabidhi mmiliki wa blog ya ignatusvero kadi
ya uwanachama wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PSPF katika hafla ya
ufungaji wa mafunzo kwa Bloggers Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es
Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema kuanzia
mwakani wizara yake itaanzisha tuzo mahsusi kwaajili ya blog za
Tanzania.
Akizungumza
wakati akifunga mkutano mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa
waendeshaji wa blog nchini, TBN jijini Dar es Salaam Jumanne hii, Nape
amesema kwa kazi kubwa ambayo blog zimekuwa zikiifanya katika
kuhabarisha umma, ni muda wa kuanza kuwatuza wale wanaofanya vizuri.
Amesema alipata wazo la kuja na tuzo za aina hiyo wakati akisafiri kwenye ndege na kuona jarida linaloelezea tuzo za blog za Kenya na kuona kuwa kuna ulazima wa Tanzania pia kuwa na tuzo hizo.
Nape amedai kuwa lengo la tuzo hizo zitakazotolewa mwanzoni mwa mwaka ujao, zitakuwa ni kwaajili ya kuzisaidia blog kuweza kuwa na ‘specialization’ katika maudhui mbalimbali.
Amesema tayari ameshaanza kuzungumza na makampuni na taasisi mbalimbali kwaajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapewa zawadi kubwa ili kuwahamasisha zaidi. Ameahidi kuwa tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi na kwamba makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini.
Post a Comment