Wawakilishi wanawake wamesisitizwa kujenga utamaduni
wa kujiongezea maarifa na ufahamu katika masuala ya utawala ili kupanua
demokrasia ndani ya Baraza la wawakilishi Zanzibar.
baraza la wawakilishi zanzibar
Akizungumza
katika siku ya mwisho ya mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wawakilishi
wanawake, Naibu spika wa Baraza la wawakilishi Mgeni Hassan Juma amesema hatua
hiyo itawasaidia wajumbe hao kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Amesema
lengo kuu la
mafunzo hayo ni
kuwajengea uwezo wawakilishi
hao katika maswala ya
mawasiliano, kujitambua hasa pale
wanapojenga hoja katika
kuwasilisha barazani lakin
pia kuweza kujiamin wakati
wa vikao
vya ndani na
nje.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kunufaika kwa kupata muamko katika masuala
ya kuchangia ndani ya vikao kutokana na kujifunza sheria na kanuni zinazolihusu
Baraza la wawakilishi.
Mradi huo
wa mafunzo ya siku 4 unaoitwa
ujengaji wa uwezo
ulioshirikisha wawakilishi wanawake
Zanzibar umedhaminiwa na shirika la umoja wa mataifa la wanawake UN
WOMEN.
Post a Comment