Imeelezwa kuwa licha ya
uwepo wa asasi za kiraia zinazotoa elimu kwa jamii kuhusu masuala yanayohusu
watu wenye ulemavu, bado baadhi ya watu wamekuwa wakiendelea kufanya vitendo
vya udhalilishaji kwa jamii hiyo.
Mkuu wa mkoa wa mjini
magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 8
kwa watu wenye ulemavu wa akili kwenye ukumbi wa Skuli ya maandalizi Saateni
mjini Unguja ambapo amezipongeza asasi hizo kwa elimu wanayoitoa kuhakikisha
masuala ya udhalilishaji hasa kwa watu wenye ulemavu yanaondoka.
Nae mwakilishi wa watu
wenye ulemavu Zanzibar Bi. Mwantatu amezitaja baadhi ya changamoto
zinazoikabili jamii ya watu wenye ulemavu wa akili nchini ni pamoja na wazazi
wengine kutokutowa huduma bora za msingi kwa watoto wenye matatizo ya akili.
Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha walimu
kutoka katika skuli za Unguja na Pemba, watu wenye ulemavu na wadau wengine.
Post a Comment