Kiasi cha sh. 25 milioni kimetengwa kwa ajili ya
kukopesha vikundi vya ushirika vilivyomo
ndani ya jimbo la Chumbuni, visiwani Zanzibar
Mwakilishi
wa jimbo hilo Mhe. Miraj Kwanza amesema lengo la kutengwa kwa fedha hizo ni
kuwasaidia wanajamii kuinua maisha yao kupitia vikundi vya ushirika.
Mhe.
Kwanza amesema tayari vikundi 56 vimepokea mafunzo ya wiki moja kutoka kwa
wataalam wa masuala ya vikundi vya ushirika Zanzibar.
Aidha amewasihi
wananchi wa jimbo la Chumbuni kuongeza ushirikiano ili kudumisha maendeleo ya
jimbo lao kupitia vikundi vyao vya ushirika.
Post a Comment