0


Waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kusheherekea sikukuu ya Krismas kwa kufanya Ibada pamoja na mambo yanayompendeza Mungu.

Akizungumza na Liwale blog Mchungaji Charles Kiyengo kutoka Kanisa la RGC Welezo amesema watu wengi wamepoteza dhana ya sikukuu ya Krisimas ambayo ni kuwahimiza waumini kufanya ibada badala yake wamekuwa wakifanya mambo kumchukiza Mungu.
Mchungaji Kiyengo amesema waumini wa dini ya Kikristo wanapaswa  kurudi katika dhana kuu ya sikukuu ya Krismasi ambayo huwahimiza waumini wake kufanya ibada,kuwajali wagonjwa  na watu wenye maisha magumu.
Nae Mchungaji Gaudance Mihungo kutoka Kanisa la Deper Life Miembeni Unguja amesema  waumini wanatakiwa kusheherekea sikukuu ya  Krismasi kwa kuungana na familia zao huku wakitafakari maana halisi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
Nae Mchungaji Philipo Kiyanda kutoka Kanisa la RGC Hanyegwamchana amesema kuzaliwa kwa Yesu Kristo  ni tukio lililotabiriwa  miaka mingi na halikuja kwa kubahatisha bali ni kuwatoa watu katika maisha yasiyo na utakaso.
Amesema Krismasi haipo kumsukuma mtu kufanya uovu bali ipo kwa ajili ya kumkumbusha mtu kufanya mambo mema na kupokea baraka kwa kuwa Krismasi ni ukombozi wa mwanadamu kutoka kwa Mungu.
Waumini wa dini ya Kikristo nchini leo wanaungana na waumini wenzao duniani kuadhimisha kuzaliwa kwa bwana na mwokozi wao Yesu Kristo takribani miaka 2000 iliyopita na Ujumbe wa krismas wa mwaka huu ni haki na amani kwa wanyonge.

Post a Comment

 
Top