Naibu
Katibu Mkuu CCM Zanzibar mh: Vuai
Ali Vuai leo amekabidhi gari aina ya Kenta
kwa Jimbo la Chumbuni ili kutatua
changamoto mbali mbali zinazowakabili jimboni
hapo.
Naibu katibu mkuu zanzibar Vuai Ali Vuai
Akikabidhi
gari hiyo jimboni hapo ambayo imetolewa na mbunge, mwakilishi na diwani wa jimbo hilo mh: Vuai amesema gari hiyo
itatumika jimboni hapo bila
ya kujali itakadi ya chama chochote.
Kwa
upande wao mbunge wa jimbo hilo mh: ussi salum pondeza na mwakilishi wake
mh:miraji mussa khamisi wamewataka wananchi wa jimbo hilo kuondoa tofauti zao
za kisiasa kwa lengo la kupeleka mbele maendeleo ya jimboni humo.
Mh mbunge wa jimbo la chumbuni Ussi Salum Pondeza (kulia)
Akisoma
Risala katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, Abrahman Abass alisema vifaa
hivyo vimetolewa na viongozi wa jimbo hilo ambao ni Mbunge, Mwakilishi na
Madiwani.
Alivitaja
vifaa vyengine vilivyotolewa kuwa ni pamoja na Dawa za binadamu kwa ajili ya
vituo vya Afya vya jimbo hilo pamoja na jezi za mpira wa miguu kwa timu za
jimbo zenye usajili wa ZFA.
ZAIDI
ya shilingi milioni 43 zimetumika kununua vifaa mbali mbali vya Jimbo la
Chumbuni Zanzibar, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Viongozi wa
jimbo hilo kwa wananchi katika Kampeni za Uchaguzi uliopita.

Post a Comment