KATIBU
wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar wa Idara ya Itikadi na
Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu amewataka Wana CCM kuendelea kuthamini mchango
wa hali na mali iliyotolewa na Waasisi wa Vyama vya ASP na TANU katika harakati
ya kuwaletea Uhuru wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Kauli
hiyo ametoa katika nyakati tofauti alipokuwa akizungumza na Wanachama wa CCM wa
Matawi wa
Chaani, Mkwajuni, Nungwi na Kijini ya
Wilaya ya Kaskazini “A” ikiwa ni mfululizo wa ziara yake ya kukagua Uhai wa
Chama Wilayani humo.
Amewataka
Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kuwa mstari wa mbele na kutumia mafanikio
na changamoto za Waasisi hao, kama njia mojawapo ya kuendeleza mapambano ya kukumbuka
na kuthamini kwa vitendo juhudi zao hizo.
Amesema
Waasisi wa vyama vya TANU na ASP walijitolea muhanga kuhakikisha Wananchi wa
Tanganyika na Zanzibar wanakuwa huru
kutoka kwenye makucha ya wakoloni wa Kiingereza na
Kisultani walozitawala kwa mabavu nchi
mbili hizo, kwa zaidi ya miaka 150
iliyopita.
Bi.
Waride amesisitiza haja kwa Wana CCM kuzidisha mashirikiano miongoni pamoja na
kubuni mbinu na mikakati madhubuti ya kiuchumi itakayosaidia kwa kiasi kikubwa
kukuza mapato ya Chama.
Ametoa
wito kwa Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na wananchi kwa
ujumla wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudumusha suala zima la amani na utulivu
uliodumu kwa miaka 53 sasa, kwa maslahi ya Taifa na wananchi wake.
Post a Comment