0


Baada ya kupisha sherehe za Krismas hii leo, Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho kwa kuchezwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi Mkoani Pwani ambapo wenyeji Ruvu Shooting watashuka dimbani kuwakaribisha washika bunduki za magereza Tanzania Prison kutoka Jijini Mbeya

Huo utakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Ruvu Shootin kucheza katika uwanja wake wa nyumbani katika mzunguko huu wa pili ulioanza kutimua vumbi novembe 17,ambapo katika mchezo wa awali Ruvu wakiwa uwanjani hapo walitoshana nguvu kwa kufungana bao moja kwa moja na Mtibwa Sugar Kutoka Wilayani Turiani Mkoani  Morogoro
Ruvu Shooting watashuka dimbani kesho kucheza mchezo wao wa kumi na saba wa Ligi kuu Tanzania bara kwakua hadi sasa ipo katika nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi, wakiwa wamecheza michezo  16, wameachwa kwa nafasi mbili na wapinzani wao Tanzania Prizoni kutokea juu, ambao wapo katika nafasi ya  7, michezo kumi na sita na point zao 22
Katika mchezo huo  Ruvu Shooting inahitaji kufanya vizuri ili ijiweke katika nafasi nzuri ya kupigania kutoshuka daraja mwishoni mwa msimu.
Tanzania Prisoni wao wanashuka dimbani  wakiwa wanakumbukumbu nzuri ya kushinda mchezo wao wa kwanza uliochezwa  Desember 18  dhidi ya Maji Maji ya Ruvuma mchezo ambao ulipigwa katika uwanja wa Sokoine Jijini  Mbeya na Tanzania Prison ikafanikiwa kushinda Goli mmoja kwa sifuri
Ligi hiyo itaendelea tena Mwaka 2017

Post a Comment

 
Top