Amesema watu hao hivi sasa wameanza kujipitisha kutaka kumrithi Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya muda na kwa hatua hiyo huenda
wakapoteza sifa.
Kauli hiyo aliitoa juzi Ikulu Dar es Salaam, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dk. Magufuli aliwaonya makada hao wanaoanza
kujipitisha kutaka urais wa Zanzibar kabla ya muda, huku akitaka Dk.
Shein aachwe afanye kazi.
“Rais Magufuli alikuwa mkali sana, hasa ilipoletwa ajenda ya hali ya
kisiasa Zanzibar, ambayo ilikuwa ikiangazia uchaguzi wa marudio na wana
CCM waliosaliti chama.
“Alisema hivi sasa wapo mawaziri ndani ya CCM wameanza kujipitisha
kutaka kumrithi Dk. Shein kabla ya wakati wake na akawaonya kuwa
wamuache afanye kazi muda wake,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kilisema kutokana na hali hiyo, Dk. Magufuli alisema kuwa
ili mtu awe rais ni lazima apitie taratibu zinazokubalika na chama na si
vinginevyo.
Mawaziri na vigogo kadhaa wanatajwa na wana CCM kwamba huenda wakajitosa
katika kinyang’anyiro cha urais wa Zanzibar mwaka 2020 wakiwamo Waziri
Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Miundombinu wa Zanzibar, Balozi
Ali Abeid Karume.
Nahodha alikuwa mmoja wa vigogo waliojitosa mwaka 2010 kuwania kuteuliwa
kuwa mgombea urais, lakini alikuwa mshindi wa tatu akipata kura 33,
nyuma ya Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na Dk. Shein
aliyeibuka mshindi kwa kura 117.
MATOKEO UCHAGUZI PEMBA
Mbali na hilo, pia katika ajenda hiyo ya hali ya kisiasa Zanzibar,
iliwasilishwa taarifa ya namna chama hicho tawala kinavyoteswa na
matokeo ya uchaguzi wa wabunge na wawakilishi kwa majimbo ya Pemba.
Kutokana na hali hiyo, juzi NEC iliagiza kuundwa kamati maalumu ya
kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na
masuala yanayohusu uchaguzi wa 2015.
Wakati hayo yakiendelea, leo Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar,
Dk. Shein, anatarajiwa kuongoza kikao cha Kamati Maalumu ya NEC.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Kamati
Maalumu ya NEC Zanzibar – Idara ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakar Jabu,
ilisema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Ofisi Kuu ya
CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Alisema kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili mapendekezo
ya wanachama wa CCM, wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge
katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani.
“Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu
ya NEC, ambacho kimefanyika leo (jana) chini ya Mwenyekiti wake Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa agenda
za kikao hicho,” alisema Waride katika taarifa yake.
Chanzo-Mtanzania
Post a Comment