Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
John Magufuli ametoa msaada wa chakula na vinywaji kama zawadi ya sikuku ya
Krismasi katika kituo cha wazee Bukumbi kilichop jijini Mwanza.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amewambia wazee hao kuwa pamoja
na kusherekea sikukuu hiyo wasisahau kumuombea Rais kwa kazi kubwa
anayoifanya ya kuliongoza Taifa.
Mkuu wa mkoa wa mwanza JOHN MONGELA
Crement Bullo ni mzee anayeishi katika
kituo hicho amesema wanaishukuru serikali kwa msaada wa chakula na kusema kuwa
kwa sasa wana chakula cha kutosha lakini tatizo linalowafanya wanarudi mtaani
kuombaomba ni kwa ajiri ya kupata hela ya kubadilisha mboga.
Naye afisa ugavi na manunuzi wa
kituo hicho Jeremiah Nyanda amesema pamoja na kumshukuru Rais wanaiomba
serikali kuwasaidia kutatua changamoto waliyonayo ya kukosa uzio pamoja na jiko
ukizingatia kituo hicho kina walemavu wa ngozi hivyo kukosa uzio ni hatari kwa
usalama wao.


Post a Comment