Jeshi la polisi mkoa
wa kusini unguja limejipanga kwa kufanya doria yenye lengo la kunusuru na
kudhibiti vitendo vya udhalishaji wa jinsia kwa watoto wanaokwenda kwenye maeneo
ya kusherehekea sikukuu za chrimasi na mwaka mpya.
Pia kamanda wa
polisi mkoa wa kusini Unguja ametoa wito kwa wananchi kwa ujumla kusherehekea
sikukuu ya krimasi na mwaka mpya kwa amani na utulivu.
Aidha amewataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mapema kwenye
jeshi hilo iwapo watagundua kunataka ama kumefanyika vitendo vya uhalifu
nchini.
Aidha
amewataka wamiliki wa nyumba za starehe walioruhusiwa wazingatie uhalali wa
matumizi ya kumbi zao.


Post a Comment