WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kukagua eneo la ujenzi wa
makazi ya askari wa Magereza unaotarajiwa kuanza baada ya wiki tatu zijazo.
Waziri mkuu wa TANZANIA KASSIM
MAJALIWA
Akizungumza na askari wa magereza kabla
ya kufanya ukaguzi huo leo Waziri Mkuu amesema ziara yake hiyo, ni ufuatiliaji
wa maagizo ya Mhe. Rais John Magufuli aliyoitoa wakati alipoenda kukagua gereza
hilo Novemba 29 mwaka huu na kupokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi
askari wa jeshi hilo takriban elfu 9 na 500 ambapo aliagiza kutafutwa kiasi cha
sh. Bilioni 10 ili kupunguza tatizo hilo.
Waziri mkuu wa TANZANIA KASSIM
MAJALIWA
Waziri Mkuu amesema amefarijika
kukuta Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wako eneo la kazi na wameanza kusafisha
eneo hilo.
Amesema katika ziara alizozifanya
kwenye mikoa mbalimbali, alitembelea magereza ya Isanga, Msalato mkoani Dodoma,
Lindi, Singida na Keko jijini Dar es Salaam na kukuta nyumba za askari hazina
viwango na kama zipo zimechakaa sana.
Awali, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa
nyumba hizo, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa amesema
wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa makazi ya askari na
kwamba jeshi hilo litafanya kazi zote zisizo za kitaalamu ili kuokoa fedha za
Serikali na badala ya kulipwa watu binafsi, fedha hizo zitatumika kuongeza
nyumba zaidi.


Post a Comment