Ligi kuu tanzania bara imeendelea kurindima katika viwanja sita, katika Mikoa tofauti tofauti hapa nchini,ambapo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dare es Salaam vinara wa ligi kuu Simba wameendelea kujidhatiti kileleni baada ya kushinda bao moja kwa duara dhidi ya Jkt Ruvu katika mchezo ulioanza majira ya saa 10 jioni ya leo Jijini Dare es Saalam
Goli hilo limepatikana katika dakika 45 lililofungwa na Muzamiru Yaasini baada ya shambulio kali lililofanywa na Simba katika dakika 44 na kusababisha wachezaji wa Jkt Ruvu kumzonga mwamuzi Hans Mabena wa Tanga aliyesaidiwa na Omar kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani kwa madai kuwa kipa wao alikua amelala chini.
Katika kipindi cha pili Simba walionekana kutawala mpira zaidi na kupelekea kulisakama lango la wapinzani wao ambapo katika dakika Dk 49, Simba walimtoa Bukungu na nafasi yake ikachukuliwa na Hamad Juma ambapo jkt ruvu nao walifanya mabadiliko katika Dk 55, Ally Billa alitoka nje na kuingia Najim Magulu
Dakika chache baadae Jkt Ruvu wakafanya mabadiliko kwa mara nyengine kwa kumuingiza Atupele Green baadaya Salim Gilla kuumia
Licha ya mabadiliko hayo lakini bado Simba waliendelea kumiliki mchezo ambapo katika dakika 62 Mo Ibrahim alitoka na nafasi yake ilichukuliwa na Jamal Simba Mnyate
Simba walienokana kutawala lango la Jkt zaidi lakini umakini waumaliziaji ulionekana kuwa mdogo zaidi katika kikosi hicho ambapo mwalimu Omog alilazimika kufanya mabadiliko mengine kwa kumtoa mkata umeme wao kutoka nchin Ghana Kotei katika dakika 79 na kuingia Said Ndemla.
Karika mchezo huo Mshambuliaji Pastory Athanas aliyesajiliwa dirisha dogo
mwezi huu kutoka Stand United akicheza kwa mara ya kwanza leo alionyesha
kiwango cha hali ya juu na kuwafurahisha wanachama na mashabiki wa Simba.
Hii leo akicheza kama mshambuliaji mbele ya lango la
JKT, Pastory aliisumbua ngome ya timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania na
kukaribia kufunga mara kadhaa.
Kwasasa Simba inakaa kileleni ikiwa
inajumla ya point 41,huku wakiwa wamecheza michezo 17 sawa na watani wao Yanga
ambao wako katika nafasi ya pili na point zao 37 huku wakicheza michezo 17.
Kikosi cha
Simba hii leo kilikuwa Kipa Mghana, Daniel Agyei alionyesha kiwango kizuri
akiokoa michomo kadhaa ya hatari na kuizuia Simba SC kuruhusu bao, Jonas Mkude,
Janvier Bukungu/Hamad Juma dk50, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda,
Method Mwanjali, Shiza Kichuya, James Kotei/Said Ndemla dk79, Pastory Athanas
na Mohamed Ibrahim/Jamal Mnyate dk62.
Na Jkt Ruvu nao kiliundwa na: Hamis
Seif, Salim Gilla, Michael Aidan, Frank Nchimbi, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon,
Edward Joseph, Hassan Dilunga, Hassan Materema, Mussa Juma/Kassim Kisengo dk80
na Ally Bilal/Atupele Green dk62.
Katika michezo mengine ya ligi kuu iliyochezwa
leo, Maji Maji walishuka Dimbani wakiwa nyumbani Dhidi ya Azam na kufungana bao
moja kwa moja,wakati Mbeya City walishuka katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya
kuwakaribisha Toto Africa ya Mwanza na
kutoka suluhu ya bila kufungana
Huko Mkoan Mtwara Ndanda ya Mtwara
0-2 Mtibwa Sugar ya Morogoro, wakati Mwadui wameshinda goli 1-0 dhidi ya Mbao
Fc ya Mwanza
Na huko kaitaba Kagera Sugar
ameshinda goli 1-0 dhidi ya Stand United
Ligi
hiyo kubwa zaidi kwa Tanzania bara itaendelea tena tarehe 26 kwa kupigwa mchezo
mmoja katika Uwanja wa Mabatini kwa kuwakutanisha wenyej Ruvu Shooting v
Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandazi].



Post a Comment