Aliyekuwa
Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo(LGTI), Emanuel Gibali na
wenzake wawili wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Wilaya ya Dodoma
kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh 12.4 milioni kutoka Manispaa ya
Morogoro.
Akisoma
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Godfrey Pius,
Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
(Takukuru), Biswaro Biswaro alisema washtakiwa hao wanakabiliwa na
makosa manne ambayo waliyafanya Septemba, 2015 chuoni hapo.
Biswaro
aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na Mkuu wa Idara ya
Utafiti ,Ushauri na Mafunzo Mafupi, Benjamen Magori na Mhasibu wa Chuo
hicho, Eliakundi Samanya.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Pius alisema dhamana zipo wazi na
kutoa masharti kuwa kila mmoja anatakiwa kujidhamini mwenyewe kwa mali
isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya Sh 2 milioni na dhamini moja
mwenye barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa.
Watuhumiwa
wote watatu wapo nje kwa dhamana baada ya kutimiza msharti ya dhamana
na kesi yao itatajwa tena januari 18, waka 2017 .

Post a Comment