Mkuu wa wilaya Joseph Mkirikiti alisalimia na wananchi wa kijiji cha NKOWE wilaya humo hivi karibuni
Fadhula Milanzi Ruangwa
Mkuu Wa wilaya ya
Ruangwa Mkoani Lindi Joseph Joseph
Mkilikiti amepiga Marufuku kwenye shughuli zinazoendana na Vigodolo kucheza
staili ya Chura na Funua Dela.
Kauli hiyo ameitoa
Leo alipokuwa anaongea na waandishi Habari .Mkuu huyo amesema kuwa katika
shughuli za Ndoa,Jando na Unyago kumekuwa kuna mziki maarufu vigodolo ambapo
kumekuwa na staili ya kuchezesha makalio maarufu Chura na ile staili ya kufunua
Dela ambapo wanawake wakiwemo wasichana wamekuwa wanajifunua
Dela na kubakia na nguo za ndani tu.
“Hii no kinyume na maadili ya mtanzania.;kwakuwa inadhalilisha
jamii na wao wenyew’alisema Mkirikiti.
Mkuu huyo wa
wilaya amemtaka Afisa Utamaduni Wa Halmashauri ya Wilaya ya
Ruangwa Hussen Mkambala kufuta vibali
vyote vya vigodolo ambavyo vitatumika vibaya kwa kufanya mambo yanayokwenda
kinyume na maadili ya Kitanzania.
Mkirikiti ameviagiza vyombo vya usalama kusimamia
jambo hili. Esha Chimbanga mkazi Wa Kijiji cha Likangara amekiri kuwapo kwa
michezo hiyo ya kucheza uchi au nusu uchi jambo ambayo yeye ameyaona kuwa
yanafaa kukemewa pia amesema kama yataachiwa yaendelee yataharibu kizazi cha
sasa na kijacho kwani tayari baadhi ya watoto wadogo wanaiga
Mkuu wa wilaya akisalimia na Diwani wa Nnowe wilayani Ruangwa
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.