Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imezindua huduma ya kuweka mfumo
maalum wa usikivu na kuwawekea watoto 16 wenye tatizo ya kutosikia hatua
iliyofanikisha kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 22 kwa kila mtoto mmoja
iwapo angepata matibabu hayo nchini India.
Akimkaribisha Katibu mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo ya jamii,wazee na watoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof.Lawrence Museru amesema mfumo huo katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Tanzania ndio nchi pekee inayotoa huduma hiyo na kusisitiza kuanzia mwezi Januari mwakani itaanza kutoa huduma za upasuaji hatua itakayosaidia serikali kuokoa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa kila mtoto mwenye tatizo la usikivu.
Akizungumza na madaktari,wauguzi na wazazi wa watoto wenye matatizo ya kusikia,Katibu mkuu wa Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, daktari Mpoki Ulisubisya amepongeza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuisaidia serikali kupunguza gharama za kugharamia matibabu ya Watanzania nje ya nchi na kuwataka wazazi kuwachunguza watoto mapema ili kugundua kama wana tatizo la usikivu.
Wakizungumza na waandsihi wa habari baadhi ya wazazi licha ya kuishukuru seikali kwa kutoa kipaumbele katika tatizo la usikivu kwa watoto,wamesema baadhi yao wamelazimika kupumzika kazini kwa zaidi ya miezi minne ili kusafiri na watoto hao kwenda nchini Iindia kwa matibabu hali ambayo imewaathiri sana kiuchumi kutokana na gharama kubwa la malazi licha ya msaada wa serikali.

Post a Comment