Kiongozi wa chama cha waandishi wa habari nchini
Misri, na wakuu wengine wawili, wamehukumiwa kifungo cha miaka miwili,
kwa kuwapa hifadhi wenzao waliokuwa wakisakwa na polisi.
Hukumu
hiyo, ambayo inaweza kufutwa wakilipa faini ya dola miasita, inafuatia
msako wa polisi kwenye ofisi ya jumuiya ya wafanyakazi mjini Cairo mwezi
wa Mei, wakati polisi wakiwasaka waandishi wa habari wawili.
Hao walishutumiwa kulalamika juu ya uamuzi wa serikali ya Misri, kuikabidhi Saudi Arabia, visiwa viwili katika Bahari ya Sham.
Post a Comment