Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi
Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna
jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi
239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa
mikopo yao.
Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa Sugu", Badru amesema kuwa ni
wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio ukapita bila kuwasilisha
taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa
masomo 1994/1995.
Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru amesema mbali na kutoa
siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa
kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1).
Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za
mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani
majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine
wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo.
Kuhusu takwimu za mikopo iliyotolewa, amesema tangu 1994/95 hadi 2015/16
jumla ya shilingi 2,595,932,575.56 zimekopeshwa kwa jumla ya wanufaika
379,179.
Amesema kati ya mikopo yote iliyokopeshwa, mikopo iliyoiva ni shilingi
1,425,708,285,046.48 kwa wanufaika 238,430 ambao tayari wamemaliza
kipindi chao cha matazamio.
Badru amesema kuwa jumla ya wanufaika wa mikopo 93,500 wamebainika na
kupelekewa ankara za madeni yao, ambapo kati yao wanufaika 81,055
wanaendelea kulipa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.