SERIKALI imesema nchini wana nafasi ya kufanya biashara ya magogo kwa
kuzalisha bidhaa nchini na hatimaye kuzisafirisha na kuziuza nje badala
ya kuyasafirisha magogo hayo kama malighafi kwenda nje ya nchi.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa uwekezaji wa misitu uliowashirikisha wadau wa Mazingira kutoka nchi 16 ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi.
“Wawekezaji wa misitu wanasema wanataka soko la mazao yao na sisi tunasema soko lipo isipokuwa watengeneze bidhaa kama vitanda, viti na samani za ndani pamoja na makaratasi na vifaa vyote vinavyotokana na miti na hiyo ndiyo itasaidia ndugu zetu kupata ajira na viwanda vitaongezeka,” alisema Profesa Maghembe.
Aliongeza, “Tukiruhusu magogo kwenda nje itakuwa kama pamba yetu inalimwa hapa na kusafirishwa halafu inatengeneza nguo na tunaletewa, lazima Viwanda vijengwe na hiyo si kazi ngumu.... Tunachotaka hapa teknolojia ya viwanda ije, wasafirishe bidhaa na si magogo.”
Alisema inakaridiwa kwamba hekta 30,000 za misitu zinapotea kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali huku zikiwa zinapadwa hekta 80,000 hadi 100,000 kila mwaka.
Alisema kuna changamoto kubwa ya uchomaji mkaa na wengine wanasafirisha nje kupitia kwa bandari bubu na hivyo misitu kupotea kwa sababu pia ya uvunaji wa misitu usio endelevu.
Alisema changamoto nyingine ni kupungua kwa vyanzo vya maji kutokana na ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa misitu, hivyo wanaongeza juhudi kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja alisema jukumu lao ni kuwaweka viongozi na wadau mbalimbali katika kuangalia maendeleo endelevu ambapo kwa sasa wanaangalia mabadiliko ya tabianchi kwa kuangalia jinsi ya kuboresha na kuendeleza misitu kibiashara.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Yutaka Yoshino alisema Idara ya Misitu nchini imekuwa ikichangia ukuaji wa uchumi nchini, lakini sekta hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi.

Post a Comment