0
Mfungwa wa Uholanzi 
Mfungwa wa Uholanzi katika gereza la Esserheem
Huku maeneo mengi ya dunia yakihangaika na magereza yaliyojaa wafungwa kupita kiasi, Uholanzi ina tatizo tofauti. Uhaba wa wafungwa.
Katika kipindi cha chini ya miaka 19, magereza yamefunga shughuli zake na mengine zaidi yamepangwa kufungwa mwaka ujao. Ni vipi hili liliwezekana - na kwa nini baadhi ya watu wanafikiri ni shida?
Harufu nzuri ya kupendeza ya vitunguu inanukia, kupitia mlilango ya mahabusu na katika jengo zima. Jikoni wafungwa wanaandaa chakula chao cha jioni. Mwanamume mmoja aliyeko upande mmoja wa jiko anakata mboga.
"Nilikuwa na miaka sita ya kujifunza sasa nina uelewa zaidi wa shughuli hii!" alisema.
Ni kazi yenye kelele kwa sababu kisu kimefungwa kwenye nyororo ndefu iliyofungwa juu.
"Hawawezi kuchukua kisu hicho mikononi ," anasema Jan Roelof van der Spoel, naibu gavana wa gereza la Norgerhaven, lenye ulinzi mkali lililoko kaskazini mashariki mwa Uholanzi. "
"Lakini wanaweza kuazima visu vidogo vya jikonikama wakitoa vitambulisho vyao ili tufahamu ni nani ana nini."
Baadhi ya wanaume hao wamefungwa kwa kufanya makosa ya ghasia na wazo kwamba watembee na visu ni suala linalotia shaka. Lakini kujifunza kupika ni moja tu ya njia ambazo gereza husaidia wafungwa kurejea katika maisha ya kawaida mara baada ya kufunguliw. KWA HABARI ZAIDI BOFYA >>HAPA

Post a Comment

 
Top