0
 Kaimu katibu tawala wilaya ya Liwale,bw. Salum Chautundu (kushoto) pia ni Mwenyekiti wa kikao cha leo cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika novemba 24 kwenye ukumbi wa John Malecela (Liwale day) kulia ni mbunge wa jimbo la Liwale,mhe. Zuberi Kuchauka.

 Baadhi ya wajumbe walioudhulia kikao cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika leo novemba 24 kwenye ukumbi wa John Malecela (Liwale day)

 Baadhi ya wajumbe walioudhulia kikao cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika leo novemba 24 kwenye ukumbi wa John Malecela (Liwale day)
 Baadhi ya wajumbe walioudhulia kikao cha kamati ya ushauri wilaya kilichofanyika leo novemba 24 kwenye ukumbi wa John Malecela (Liwale day).

Kikao cha kamati ya ushauri wilaya ya Liwale mkoani Lindi kimefanyika leo novemba 24 katika ukumbi wa John Malecela kiongozwa na mwenyekiti,Bw Salum Chautundu na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali ikiwemo wakuu wa idara na viongozi wa siasa.

Katika kikao hicho wajumbe waliweza kujadili,kushauri na hatua za kukabiliana na changamoto katika masuala mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016/2017,ununuzi wa zao la korosho msimu 2016/2017,hali ya chakula,idara ya elimu,taarifa ya kudhibiti na kupambana na rushwa.

Usalama wa raia na mali,jeshi la polisi wilaya ya Liwale lina makao makuu yake katika mji wa Liwale likiwa na jengo moja la kituo cha polisi katika kata ya Liwale mjini baadhi ya wajumbe walishauri ipo haja ya kuongeza vituo vya polisi kwenye maeneo ya kibiashara kama kwenye kata ya Kibutuka na kata ya Lilombe maeno haya yakiwa na  mwingiliano wa watu mbalimbali wanaofanya shughuli za kiabishara.
 
Sekta zingine zilizojadiliwa ni utafiti,udhibiti na takwimu, pamoja na taarifa ya shirika la umeme (Tanesco),wilaya ya Liwale inapata umeme kwa kutumia njia ya Genetor kuna jenereta mbili aina WARTISILA-424 ambapo kila moja ina uwezo wa kutoa kilowatt 424 na kwa mashine mbili zina uwezo wa kuzalisha jumla ya kilowatt 848 wakati mahitaji ya juu ya umeme katika mji wa Liwale ni 450kw.

Umeme wa REA awamu ya pili sehemu zilizoingizwa na kkatika mpango huo wa REA na awamu ya pili Mangirikiti,sekondari ya Anna Magoha,Kipule kijijini,Kipule Magereza,Likombora,sekondari ya Mihumo,Mihumo-I,Mihumo-II,Mikunja,Kiangara,Kibutuka,Nangano na Turuki.

Pia kuna vijiji 53 vya wilaya ya Liwale vilivyopangwa  kwa ajili kupata umeme wa REA awamu ya III,kuanzia mwaka 2016/2017 mpaka mwaka 2020/2021

Post a Comment

 
Top