Wafugaji
nane akiwemo diwani wa kata ya Businde wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera
washikiliwa na jeshi la polisi kwa saa 24,huku mifugo inayomilikiwa na
watendaji wa serikali yaondolewa kwa nguvu katika shamba la muwekezaji
Kitengule baada ya kukiuka sheria,taratibu na kanuni za uwekezaji ili
kupisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baada
ya wafugaji kushikiliwa na jeshi la polisi huku mifugo 268 ikifungiwa
bila malisho kwa siku nne,mbunge wa jimbo la Karagwe Mh.Inosent
Bashungwa akalazimika kuingilia kati mgogoro uliyoibua siri kubwa
iliyofichika ikiwemo mifugo iliyokufa kwa kukosa malisho ikipoteza
maisha na kufukiwa ardhini .
Baada
ya sakata hilo meneja wa ranchi ya Kitengule Bw.Lebahati Emmanuel kwa
kushirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Karagwe wakalazimika kuachia
huru mifugo na watuhumiwa ambao wamesema kuwa migogoro ya kukamatwa kwa
wafugaji wa kata ya Kihanga mara kwa mara huku wakitozwa faini ya
shilingi 26500 kwa kila mfugo mmoja ambapo zaidi ya shilingi milioni 200
zimetozwa katika kipindi cha miezi sita.