Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya
siku 10 jijini Dar es salaam ambapo Jumatano hii akiwa wilayani Ilala
amesema hataweka saini katika nyaraka za ardhi hadi zipitie na Taasisi
ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Akiongea na watumishi wa Halmashauri wa Manispaa Ilala, RC Makonda
amesema watumishi wengi wa ardhi wasiowaaminifu wamekuwa wakisababisha
migogo mingi ya ardhi.
“Kuanzia sasa sitaweka sahihi katika nyaraka zozote za ardhi
zitakazofika ofisini kwangu hadi zipitie Takukuru zichunguzwe nimegundua
kumekuwa na usanii katika uuzwaji wa viwanja,”alisema.
Makonda aliongeza kuwa anazo nyaraka za watendaji waliokuwa wakifanya
uchakachauji huku akiwataka watendaji hao kufanya kazi na watu
waridhike.
Alisema wataalamu wa kupima ardhi huacha maeneo na kudai kuwa ni meneo
yenye bonde au mto huku baadae wakiyauza au hata kudai vimeisha na
baadaye kuyatumia kwa manufaa yao na wakati mwingine maofisa hao
kubadilisha mafaili ili wauze kwa watu tofauti.
Kutokana na hali hiyo, aliwatahadharisha maofisa ardhi na mipango miji
wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwa kutoa taarifa za uongo
katika hatua ya upimaji ardhi, uthamini na utoaji fidia kwa wananchi
ambao huuza kwa watu zaidi ya mmoja na kusababisha migogoro usioisha kwa
wananchi.
“Sitakubali kukaa na watumishi wa vigogo wasioweza kufanya kazi kutatika
mkoa huu ,ninafahamu watumishi waliofika Dar es Salaam kwa vimemo
ukiuliza ameletwa na kigogo yupo Tamisemi nitawangoa tu,”alisema.
Mkuu huyo bado anaendeleza na ziara yake katika sehemu mbalimbali za wilaya ya Ilala.
Post a Comment