Aliyekuwa nyota wa
timu ya soka ya Cameroon Samuel Eto'o huenda akahukumiwa kifungo cha
miaka 10 jela baada ya waendesha mashtaka kumhusisha na kashfa ya
kukwepa kulipa ushuru.
Huenda pia akalipa faini ya zaidi ya Euro milioni 18.
Kulingana
na ripoti mchezaji huyo wa zamani wa Cameroon pamoja na mshauri wake
Josep Maria Mesalles wameshtumiwa kwa kulinyima taifa la Uhispania Euro
milioni 3.8 kutoka mwaka 2006 hadi 2009,wakati alipoichezea klabu hiyo
ya Barcelona.
Mchezaji huyo atajiunga na Neymar na Messi,wote wakiichezea Barcelona ambao wanakabiliwa na mashtaka kama hayo.
Kashfa
inayomuandamana Eto'o inashirikisha madai ya kuhamisha haki za matumizi
ya picha yake katika kampuni za Uhispania na Hungary ili kukwepa
kulipa kodi, katika mikataba iliodhinishwa kama vile makubaliano yake na
kampuni ya jezi za michezo Puma.
Waendesha mashtaka waliwasilisha
malalmishi dhidi ya mchezaji huyo ,lakini naye akatoa taarifa
inayolaumu swala hilo kuwa ''uonevu na ushauri wa kifisadi''.
Eto'o
ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Uturuki ya Club
Antalayaspor,anaaminika kutolipa fedha alizodaiwa hatua ambayo
imesababisha kuanzishwa kwa mashtaka hayo.
Post a Comment